Rukwa
imeanza vizuri michuano ya Copa Coca-Cola kwa vijana wenye umri chini ya miaka
15 baada ya leo kuichapa Katavi mabao 4-0 katika mechi iliyochezwa Uwanja wa
Shule ya Sekondari Iyunga jijini Mbeya.
Mabao ya
washindi yalitiwa wavuni na Tumaini Boniface dakika ya 13 na 65, Francisco
Mkanga akipachika la pili dakika ya 29 wakati la mwisho lilifungwa dakika ya 75
na Innocent Ahombile.
Katika kituo
cha Zanzibar, wenyeji Mjini Magharibi imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya
Kaskazini Pemba kwa mabao ya Faisal Salum na Masoud Mohamed.
Mechi ya
pili katika kituo hicho ilikuwa kati ya Kusini Pemba na Kusini Unguja. Bao
pekee lililofungwa na Othman Abdallah lilitosha kuipa ushindi wa 1-0 timu ya
Kusini Pemba.
Boniface
Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)