Na Dina
Ismail
WAKATI
mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara unatarajiwa kuanza leo, dirisha dogo la
usajili kwa timu shiriki linafungwa rasmi lilifungwa rasmi juzi huku tukishudia
kila timu ikijaribu kufanya mabadiliko.
Kwa wiki
kadhaa tumekuwa tukisikia habari za usajili wa wachezaji mbalimbali ambao
wanadaiwa kuachwa ama kuhitajiwa na timu hizo.
Kila timu
ilikuwa katika harakati za kusajili wachezaji ambao inadhani uwepo wao
utaziwezesha timu zao kufanya vema katika ligi hiyo na michuano mingine na
hatimaye kutwaa ubingwa.
Zoezi la kuacha au kusajili mchezaji linafanywa na
viongozi wa timu wakifuata mapendekezo ya makocha wa timu husika.
Lakini
shughuli inakuja kipindi cha Ligi kwani makocha wanashindwa kuwa ‘fair’ katika
matumizi ya wachezaji katika michezo
mbalimbali.
Hii ina
maana kwamba, makocha ndio waliowataka wachezaji hao wasajiliwe katika timu
zao, lakini matokeo hushindwa kuwatumia
ipasavyo hivyo kuonekana mizigo.
Kwamba,
kocha alimuona mchezaji fulani anafaa na akaagiza asajiliwe na tena wengine
huasajiliwa kwa kiasi kikubwa cha fedha lakini na baada ya kuanza kwa ligi
kocha anashinda kumtumia.
Kuna baadhi
huwa na bahati kwa kuwa mchezaji chaguo la kwanza msimu mzima, wengine hujikuta
mchezaji wa akiba na wengine sasa huishia mazoezini tu.
Sasa hali ya
kusajili mchezaji na kutomtumia ni kama na ufujaji wa pesa na pia kuua kipaji
cha mchezaji.
Kwani, ni
bora usajili wachezaji wachache ambao unaamini watakufaa katika ligi na pesa
nyingine itumike kwa matumizi mengine au kumsajili mchezaji ambaye atapata
nafasi ya kucheza na kuendeleza kipaji chake.
Wenzetu nchi
zilizopiga hatua tumeona wachezaji wakicheza kwa kupiokezana yaani hakuna
wasugua benchi wa kudumu na ndio maana wanapata mafanikio makubwa.
Lakini kwa
hapa Tanzania naweza kusema makocha ndio wanaua vipaji vya wachezaji kwani
naamini kuna wachezaji ni wazuri tu tunawaona kwenye mazoezi lakini hawapewi
nafasi sana wakibahika kucheza ni mchi za kirafiki.
Mpira ni
ajira, kama mchezaji hafai ni bora kumuacha aende sehemu inayomuhitaji akacheze
na maisha yaendelee kuliko kumsugulisha benchi na matokeo yake hata kipaji
kinaishia benchi;ndiyo mchezaji hata kama anakipaji kikubwaa akikaa benchi sana
anajikuta anapoteza mwelekeo.
Mchezaji
amepambana mpka kufikia hatua ya kucheza ligi kuu bara, anasajiliwa na kupewa
kitita kizuri tu, lakini mwisho wa siku anashindwa kutimiza wajibu wake sababu
ni kocha kutompanga.
Ifikie
mahali makocha nao wawe na roho za kibinadamu kwani kama nao wangefanywa hivyo
hii leo wangekuwa makocha?
Nadhani
tutarajie mabadiliko ya upangaji wa vikosi katika mzunguko huu wa pili uwe wa haki na usawa na si upendeleo kama
inavyodhaniwa ili kuendeleza na kukuza vipaji.
Kuna timu
zimepandisha wachezaji vijana ni vema wakapewa nafasi za kucheza mara moja moja
ili kuwapa uzoefu kwani bila kufanya hivyo watatoa wapi uzoefu.
Kila la heri
makocha wa timu shiriki, George Lwandamina (Yanga), Joseph Omog (Simba), Ali
Bushir (Mwadui), Suleiman Matola (Nanda Fc), Ettiene Ndalyagije (Mbao Fc),
Mecky Mexime (Kagera Sugar), Kinnah Phiri (Mbeya City) na Athuman Bilal (Stand
United).
Pia wapo
Salum Mayanga (Mtibwa Sugar), Zeben Hernandez (Azam Fc), Kally Ongala
(Majimaji), Hamimu Mahadh (Tz Prisons), Fernando Jose Bernado Tavares ( African
Lyon),Jurgen Seitz (Toto African) na
Malale Hamsini (Ruvu Shooting).