Na Dina Ismail
LICHA ya uongozi wa Simba kutaka kumrejesha
mshambuliaji wa kimataifa Mganda
Emmanuel Okwi, kocha mkuu wa timu hiyo, Mcameroon Joseph Marius Omog hajakubaliana na hilo.
Habari za kuaminika kutoka klabu ya Simba zinaeleza kwamba,
Omog kabla ya kuondoka alipendekeza majina ya wachezaji ambao anataka
wasajiliwe na katika hiyo orodha hakukuwa na jina la Okwi.
Imeelezwa kwamba katika ripoti ya Omog, amepanga kuleta kipa
na mshambuliaji kutoka nchini Ivory
Coast kwa ajili ya kukiimarisha kikosi cha timu hiyo katika mzunguko wa pili wa
ligi kuu bara.
Omog ambaye alikwenda likizo
kwao baada kumalizika kwa
mzunguko wa pili ulioiacha Simba katika nafasi ya kwanza, anatarajiwa kurejea
nchini wakati wowote kuanzia sasa kwa ajili ya kuendelea kukinoa kikosi chake.
Simba ambayo ilimuuza Okwi mwaka juzi kwa dau la dola 100 katika
klabu ya Sonderjiske ya Denmark. ilipanga kumrejesha Okwi kwa dau la dola za Marekani 120,000 ( zaidi
ya Sh milioni 240).
Hata hivyo, habari zinaeleza kwamba, licha ya kocha
kutompendekeza Okwi katika usajili wake, uongozi wa Simba umeona dau lake ni kubwa ukilinganisha na kiwango
alichonacho kwa sasa.
“Haiwezekani Okwi
kununuliwa kwa gharama hiyo, yaani tumuuze kwa dola 100 halafu tumnunue kwa
dola 120 kwa kiwango gani zaidi, kwanza kocha hajamtaka na amepanga kuleta mshambuliaji mahiri kutoka
Ivory Coast, alisema kiongozi huyo
Okwi alipata kujiunga
Simba kwa mara ya kwanza mwaka 2010 na kuiwezesha kutwaa mataji kadhaa kabla ya
mwaka 2013 kuzwa Etoile du Sahel ya
Tunisia dola 300,000.