Mkurugenzi wa Vijana wa Taasisi ya Zanabu Mgonja (ZAM Foundation), (kushoto) akipeana mkono kutoka kwa Mohammed Zia (Mwanaharakati wa Marekani) wakati wa makabidhiano ya Pampu 2 za kisasa,kwa ajili ya vijana wa Taasisi hiyo, Makanya Pare. Katikati anayeshuhudia ni Shaban Mkanza (Mwenyekiti-Mtendaji).Makabidhiano hayo yalifanyika jana jijini Dar es Salaam.
TAASISI ya kijamii ya Zainabu MGonja(ZAM-Foundation) ya Mjini Moshi, jana imekabidhiwa pump mbili za kisasa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji kutoka kwa Mwanaharakati wa Marekani.
Makabidhiano hayo yalifanyika jana jijini Dar es Salaam, ambapo mwanaharakti huyo kutoka Marekani, Mohammed Zia, aliguswa na hali ya vijana wa Moshi Pare na kuamua kuchangia pampu hizo.
Aidha, Mkurugenzi wa Vijana wa taasisi hiyo, Hassan Ngoma alishukuru kwa msaada huo na kusema kuwa vitakuwa chachu kwa vijana wa taasisi hiyo kwani itawasaidia kuinua vipato vyao na kuachana na mambo ya kukaa vijiweni.
“Vijana wa taasisi yetu watafaidika na mradi huu, hasa maisha ya jamii ya Pare iliyo katika lindi la umasikini licha ya fursa nyingi zinazowazunguka ikiwemo ya kilimo’ alisema Ngoma.
Kwa upande wake, mwanaharakati huyo alisema kuwa, ataendelea kuimalisha uhusiano wake na taasisi hiyo wa mara kwa mara ilikuleta maendeleo kwa vijana wote.
“Nitajitahidi kila hatua ilikufanikisha vijana wa Pare wakiendelea, nitakaporudi nyumbani nitaendeleza harambee za kuchangia misaada kwa jamii” alisema Zia.
Taasisi hiyo ya ZAM Foundation, inajishughulisha na mambo ya kijamii huku makao yake makuu yakiwa mkoani Kilimanjaro,Moshi Wilaya ya Same tarafa ya Makanya.