YANGA imezidi kuchanja mbuga katika ligi kuu ya Vodacom hatua ya lala salama baada ya kuishinda Polisi Dodoma kwa mabao 2-0.
Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, mabao ya Yanga yote yalipachikwa na mshambuliaji wake wa kimataifa kutoka Zambia, Davies Mwape.