EXIM BANK YAAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI


 Na Mwandishi Wetu
Benki ya Exim imeahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika mikakati
mbalimabli ya kuinua uchumi wa nchi.
Hayo yalisemwa jijini jana na Meneja Mkuu wa benki hiyo, Bwana Dinesh Arora.
Alikuwa akizungumzia ufadhili wa benki hiyo kwenye mkutano wa uwekezaji Afrika
uliofanyika jijini katikati ya mwezi huu na kuhudhuriwa na maraisi watano kutoka
nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki na wajumbe zaidi ya 900 kutoka sehemu
mbalimbali duniani.
Alisema kuwa sekta binafsi inao wajibu mkubwa wa kuisaidia serikali kuinua
uchuni na hivyo kuboresha maisha ya Watanzania.
 “Exim Benki iliona fahari kubwa kufadhili mkutano huu ambao ulikuwa una lengo
la kuonyesha utajiri wa rasilimali za nchi na pia kufungua fursa za kibiashara”,alisema.
Bwana Arora alisema kuwa Benki ya Exim itaendelea kusaidia fursa kama hizo ili
kuwawezesha Watanzania wengi zaidi kuweza kupata nafasi ya kukutana na
wafanyabiashara kutoka sehemu nyingine za dunia.
Alisema kuwa benki yake ina wajibu mkubwa wa kuendelea kuisaidia uchumi wan chi
kukua.
Alisema kuwa ili wajasiriamali wa Kitanzaniia waweze kukua kibiashara na  kutoa
mchango mkubwa zaidi kwenye uchumi,lazima ziwepo juhudi za makusudi za
kuwakutanisha na wawekezaji kutoka Afrika na duniani kote.
 “Tunaamini kuwa maendeleo ya benki yetu yanategemea sana mafanikio ya jamii
yetu tunakofanyia kazi”alisema.
 Alisema pamoja na biashara benki hiyo ina jukumu la kuchangia shughuli
mbalimbali za kijamii na kwamba Ujasiriamali ni miongoni mwa sekta
zinazochangiwa kwa nguvu na benki husika.
“Tumekuwa tunafanya biashara ya kibenki kama jukumu letu kuu lakini pia tumekuwa na majukumu mengine kwa jamii inayotuzunguka hivyo udhamini wetu katika TEYA ni miongoni mwa utekelezaji wa majukumu hayo na kwamba Ujasiriamali tunauangalia kwa namna ya kipekee,” alisema
 Aliongeza kuwa katika kutambua umuhimu wa sekta ya hiyo,hivi karibuni wamefungua
 akaunti mpya ya Tumaini maalumu kwa ajili ya Wajasiriamali wanawake.
Alifafanua kuwa pamoja na wengine wanawake ni mhimili mkuu wa shughuli za
kijamii katika familia nyingi za kitanzania hivyo benki hiyo imeona ipo haja ya
kipekee kuwawezesha ili nao waweze kumudu majukumu yao kwa ufanisi.
Kuhusu tuzo hiyo alisema ni changamoto ya kutosha kwa Wajasiriamali nchini
katika kuhakikisha shughuli wanazozifanya zinakuwa na tija kwao binafsi na taifa kwa ujumla.
“Akaunti ya Tumaini ni maalumu kwa ajili ya Wajasiriamali Wanawake na hii
inaonyesha jinsi tunavyoijali sekta hii lakini pia tuzo hii ni changamoto kubwa
kwa wahusika kwani itawasukuma kufanya shughuli zenye tija,” alisema Bwana
Arora.
TEYA imelenga kutambua kazi za Wajasiriamali katika nyanja mbalimbali kutokana
na mchango wao katika pato la taifa na ukuaji wa uchumi lakini pia kutoa
changamoto ya ushindani kwa wahusika na sekta ya kibiashara kwa ujumla.
 TEYA 2011 ilizinduliwa rasmi Machi 15 mwaka huu na inatarajiwa kutolewa baadaye
Novemba ambapo Raisi Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Post a Comment

Previous Post Next Post