KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE 'TWIGA STARS' HIKI HAPA


Kocha wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanawake (Twiga Stars), Charles
Boniface ametangaza majina ya wachezaji 26 watakaoanza mazoezi Aprili 11 mwaka
huu kwa ajili ya mechi yao ya mchujo ya michezo ya Afrika (All Africa Games)
dhidi ya Sudan.
Wachezaji walioitwa ni Asha Rashid (Mburahati Queens), Neema Jacob (Simba
Queens), Sophia Mwasikili (Sayari), Fadhila Hamad (Uzuri), Irene Matowo
(Mburahati Queens), Hellen Tolla (JKT), Mwanahamisi Shurua (Mburahati Queens),
Fatuma Jawadu (Sayari), Fatuma Swalehe (Simba Queens), Maimuna Mkane (JKT),
Pulkelia Charaji (Sayari), Fatuma Makusanya (Simba Queens) na Mwanaidi Tamba
(Mburahati Queens).
Wengine ni Fridiana Daudi (JKT), Fatuma Salum (Mburahati Queens), Mwajuma
Abdillah (Tanzanite), Mariam Fakil (Tanzanite), Mwasiti Selemani (Tanzanite),
Aziza Lugendo (Mburahati Queens), Suzana Komba (TMK), Rukia Hamisi (Evergreen),
Pendo Juma (Evergreen), Zena Khamis (Mburahati Queens), Tatu Said (Umonga
Sekondari, Dodoma), Mwanaidi Khamis (Uzuri Queens) na Zena Said (Uzuri Queens).
Kwa siku kumi za kwanza, Twiga Stars itafanya mazoezi Uwanja wa Karume kwa
wachezaji kutokea nyumbani (off camp) na baada ya hapo itaingia rasmi kambini
Aprili 20 mwaka huu.
Twiga Stars itacheza mechi yake ya kwanza ugenini Aprili 30 mwaka huu, wakati ya
marudiano itachezwa Mei 15 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Twiga Stars ikiitoa
Sudan itakuwa imefuzu kwa michezo ya All Africa Games ambayo itafanyika Septemba
mwaka huu jijini Maputo, Msumbiji.

Post a Comment

Previous Post Next Post