MSAFARA
wa watu 25 wakiwemo wachezaji na viongozi wa timu ya Kiyovu ya Rwanda unatarajiwa kuwasili kesho tayari kwa mechi ya marudiano ya kombe la Shirikisho dhidi ya Simba itakayopigwa Jumapili katika dimba la Taifa.
Ofisa Habari wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema kitafikia katika Hotel ya Wanyama iliyopo Sinza
Jijini Dar es Salaam tayari kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo huo.
Aidha, beki wa timu hiyo Victor Costa ambaye alikuywa anakabiliwa na malaria ameshapona na jana aliripoti katika kambi ya timu hiyo.