MSAFARA wa Yanga utaondoka alfajir ya kesho kwenda Cairo Misri tayari kwa mechi yake ya marudiano ya ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Zamalek ya huko utakaopigwa Machi 4.
Hata hivyo katika msafara huo watakosekana nyota wake kadhaa wakiwemo kipa Mghana Yaw Berko na Rashid Gumbo.
Wachezaji watakaoondoka ni pamoja na Shaban Kado, Shadrack
Nsajigwa, Athuman Iddy ‘Chuji’, Juma Seif, Nurdin Bakari, Chacha Marwa, Godfrey
Taita, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Omega Seme, Davies Mwape, Pius Kisambale,
Hamis Nombo, Oscar Joshua, Haruna Niyonzima, Jerry Tegete, Job Ibrahim, Stefano
Mwasyika, Kenneth Assamoh na Shamte
Ally.