PRESS RELEASE
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
15 MACHI 2012
MABADILIKO YA KALENDA YA MASHINDANO YA UREMBO YA DUNIA:
Katika mkutano wa mawakala wa wanaoandaa mashindano ya urembo kutoka nchi mbalimbali duniani uliofanyika London Uingereza mwezi Novemba 2011, Tulijulishwa mabadiliko ya Kalenda ya mashindano ya urembo ya dunia. [Miss World.]
Mashindano ya urembo ya Dunia yanatarajia kufanyika mwezi August 2012 nchini China, badala ya mwezi Novemba/ Desemba kama ilivyozoeleka, ambapo washiriki kutoka nchi mbalimbali watatakiwa wawe wamefika nchini China mwezi Julai 2012.
Kutokana na hali hiyo tunalazimika kubadilisha kalenda ya mashindano yetu kama ifuatavyo:-
1. Tutatuma Mwakilishi atakayeshiriki mashindano ya urembo ya Dunia Miss World 2012.
2. Mwakilishi huyo atapatikana kwa njia ya usaili. Ambapo warembo watakaojitokeza
katika usaili huo watafanyiwa mchujo na kupatikana idadi ya warembo 10 watakao
panda jukwaani katika tafrija ndogo ili kumpata Mwakilishi ambaye atabeba Bendera ya
Tanzania katika Fainali za Mashindano ya urembo ya Dunia 2012.
3. Tunaomba warembo wote wenye sifa na nia ya kushiriki katika mchujo wa usaili
wawasiliane na ofisi zetu au Mawakala wete popote Tanzania kupata maelezo zaidi.
Mchakato wa mashindano ya Redds Miss Tanzania 2012 katika ngazi zote utaendelea kama kawaida na Mshindi wa Redds Miss Tanzania 2012 atawakilisha nchi yetu katika Fainali za Mashindano ya urembo ya Dunia mwaka 2013, akiwa na muda wa miezi [7] saba ya maandalizi.
Hii inakidhi haja na maoni ya Wadau wa fani ya urembo ya kumpa muda wa kutosha Mrembo wa Taifa kujiandaa vya kutosha kabla ya kushiriki Fainali za dunia.
Lundenga
HASHIM LUNDENGA.
MKURUGENZI.
|