SHETANI LAUAWA BILBAO


BILBAO, Hispania
KLABU ya Athletic Bilbao imeishughulikia tena Manchester United na kuonyesha kwamba wanastahili ubingwa wa Europa League kufuatia ushindi mwingine wa mabao 2-1 usiku wa jana na kutinga Robo Fainali.
Kikosi cha makinda wa Basque, walianzia pale walipoishia kwenye ushindi wa 3-2 katika mechi ya kwanza kwa Fernando Llorente na Oscar de Marcos kufunga mabao mengine jana.
Wayne Rooney alifunga la kufutia machozi dakika ya 81 na kuiacha klabu hiyo ya Hispania isonge mbele kwa ushindi wa jumla wa 5-3.
“Sifikirii kama tutalalamikia matokeo haya,” alisema Ferguson. “Najaribu kuuchambua msimu huu (kwa Ulaya) kuufananisha na misimu mingine ni mgumu mno. Umekuwa ni mwaka wa maajabu.”

Post a Comment

Previous Post Next Post