KAMATI
ya Utendaji ya Chama cha Soka Mkoa wa Pwani (COREFA), imemteua mwandishi wa
gazeti la Tanzania Daima na Radio Clouds FM, Victor Masangu, kuwa msemaji mpya
wa chama hicho.
Akizungumza
mara baada ya kufanyika kwa uteuzi huo, Katibu Mkuu wa COREFA, Riziki Majala,
alisema kwamba kamati imeamua kumteua Masangu, kutokana na mchango wake na
uwezo alionao katika kuleta maendeleo ya mchezo wa soka ndani ya Mkoa wa Pwani.
“Sisi kama kamati ya utendaji, katika
kuhakikisha kwamba masuala mbalimbali ambayo tutakayokuwa tukiyajadili
yanafikishwa kwa jamii nzima, hasa wapenzi wa mchezo wa kandandana, ndiyo maana
tukaamua kumteua Masangu awe ndiye msemaji wa chama,” alisema Majala.
Majala
aliongeza kuwa, pamoja na uteuzi huo, Masangu ndiye atakayekuwa Mwenyekiti wa
kamati ya kudumu ya habari na uenezi, ambapo Makamu wake ni Ben Komba, huku
wajumbe ni Alex Luambano na Shafii Dauda.
Katibu
huyo alifafanua kuwa, msemaji wa zamani, Masau Bwire, ameteuliwa kuwa
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya COREFA, makamu wake ni Mathew Shayo na
wajumbe ni Mohamed Amiri, Haji Manara na Nicholous Makini.
Kwa
upande wa Kamati ya Nidhamu, Mwenyekiti ni Shujaa Sachore, Makamu Peter
Hokororo na wajumbe ni Ally Abdalah, Musa Athumani na Mustapha Julius.