RAGE ALILIA MGAO WA SUPERSPOT KOMBE LA KAGAME



MWENYEKITI wa SImba Alhaj Ismail Aden Rage awalitaka baraza la vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuvipatia mgao wa fedha za udhamini wa michuano ya kombe la Kagame kutoka kituo cha Televisheni cha Super Sport.
Rage alisema hayo juzi katika hafla ya utoaji tuzo za washindi wa ligi kuu ya Vodacom  2011/2012 zilizofanyika katika hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam.
Alisema kutokana na maandalizi ya timu shiriki kuhitaji fedha itakuwa ni vema iwapo Cecafa itawafikiria kuwapa hata kidogo sehemu ya mgao huo.
"Tunawaomba viongozi wa Cecafa kutugawia chochote kitakachopatikana kutokana na udhamini wa Supersport katika michuano ya Kagame,"alisema Rage.
Michuano hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Julai 14 jijini Dar es Salaam ambapo Tanzania itawakilishwa na mabingwa watetezi Yanga, Simba na Azam Fc.
Yanga itafungua pazia la michuano hilo kwa kucheza na julai 14 huku Simba itakwaana na Atletico, huku Simba itatupa karata yake ya kwanza Julai 16 kwa kucheza na URA ya Uganda.

1 Comments

  1. "Tunawaomba viongozi wa Cecafa kutugawia chochote kitakachopatikana kutokana na udhamini wa Supersport katika michuano ya Kagame,"

    Ujumbe huo tujue kuwa sasa mpira ni ajira, na ajira ni gharama, ....tupo pamoja mtu wangu

    ReplyDelete
Previous Post Next Post