KOCHA Mkuu wa Simba, Mserbia
Milovan Cirkovic amesema ubovu wa kikosi chake unatokana na pengo la nyota wake
wawili, mshambualiaji wa kimataifa wa Uganda Emmanuel Okwi na marehemu
Patrick Mafisango.
Hatua hiyo inafuatia Okwi
kuwa katika majaribio nchini Australia
na Mafisango ambaye alifariki dunia usikua wa kuamkia Mei 17 jijini Dar es
Salaam kwa ajali mbaya ya gari.
Milovan alisema itachukua muda kupata mbadala wa wachezaji hao
hasa ikizingatiwa kuwa kikosi chake cha sasa kina wachezaji wengi wageni, hivyo
kushindwa kucheza kitimu.
Alisema uwepo wa Okwi na
Mafisango katika kikosi cha msimu uliopita, kulichangia kwa kiasi kikubwa
mafanikio ya timu hiyo ikiwemo kutwaa ubingwa wa ligi kuu bara, hivyo
anachofanya kwa sasa ni kukijenga kikosi chake ili kiwe katika mfumo mmoja na
kwa bahati nzuri mwelekeo wake
unaonekana sasa.