SUPER LIGI YA BANC ABC KUANZA AGOSTI 4


 Mkurugenzi wa masoko na matukio wa TFF Jimmy Kabwe akisaini mkataba wa makubaliano ya udhamini wa michuano ya Banc ABC SUP8R Soccer Tournament 2012 inayodhaminiwa na banc ABCkulia kwake ni katibu mkuu wa TFF Angetile Osiah, Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo Boni Nyoni na Mkuu wa Idara ya fedha ya benki hiyo, Mwalimu Zubery.
Osiah akibadilishana hati na Nyoni

TIMU nane toka Tanzania Bara na Visiwani zinatarjiwa kushiriki katika michuano maalum inayokwenda kwa jinala ‘Banc ABC SUP8R Soccer Tournament 2012’ inayotarajiwa kutimua vumbi Augusti 4 hadi 18.
 Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Angetile Osiah amesema leo kwamba lengo la michuano hiyo ni kuzipa makali timu shiriki kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi.
Alisema michuano hiyo itakayohusisha timu tatu bora kutoka Tanzania Bara, timu tatu bora kutoka Visiwani na timu moja iliyopanda katika pande hizio, itachezwa katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Dar es Salaam na Zanzibar.
 Alisema timu hizo zitakuwa katika makundi mawili na hakutakuwa na mechi ya kusaka mshindi wa tatu zaidi ya kuwepo kwa zawadi kwa timu itakayotwaa ubingwa tu na tayari wameshaziandikia barua za kuzitaarifu kuhusiana na michuano hiyo.
 “Nadhani hii ni nafasi nyingine kwa timu kuonyesha ushindani katika michuano hii, pia pamoja na kujiandaa kwa msimu mpya wa ligi, makocha wa timu shiriki wataweza kujua kiwango kilichopo kwenye timu zao na kama kuna kasoro warekebishe kabla ya kuanza kwa ligi,”alisema.
Banc ABC ambayo imedhamini michuano hiyo kwa miaka mitatu, kupitia kwa mkurugenzi wake Mkuu Boni Nyoni alisema wameamua kuandaa michuano hiyo ili kuunga mkono jitihada za maendeleo ya soka hapa nchini.

Post a Comment

Previous Post Next Post