KAMPUNI ya Wazalendo
Bright Media kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ipo kwenye mchakato wa
kumpata mwanasoka bora wa mwaka 2012.
Tuzo hizo
zinajulikana kwa jina la Wazalendo Best footballer of the Year Awards, ambapo
washiriki wanaoingia kwenye kinyang’anyiro hihi ni Watanzania ambao wanacheza soka kwenye Ligi
Kuu ya Tanzania Bara.
Kwa upande wa wageni
wanaocheza Tanzania watakuwa
na tuzo yao
maalum ya mwanasoka bora wa kulipwa, ambayo ipo kwenye orodha ya tuzo 11
zinazowaniwa na wanasoka.
Tuzo hizo 11 ni pamoja na kipa, beki, kiungo,
mshambuliaji, mchezaji anayechipukia, mchezaji mkongwe zaidi kwenye ligi,
mchezaji bora wa kigeni, mwanasoka bora kwa wanawake, tuzo ya heshima katika
maendeleo ya soka la wanawake, tuzo ya
heshima kwa wachezaji wa zamani pamoja na tuzo ya mwanasaisa aliyesaidia katika
maendeleo ya michezo Afrika.
Madhumuni ya kuandaa
tuzo hii ni kuongeza ushindani kwenye ligi ya Tanzania Bara, pamoja na timu za
taifa jambo litakalofanya kila mchezaji kujituma zaidi kulingana na majukumu
analiyonayo kwenye timu.
Ni imani yetu kwamba
hatua hii itaongeza uwajibikaji na utelekezaji wa majukumu kwa moro pia
itaongeza moyo wa uzalendo kwa wachezaji wa kitanzania kwenye timu za taifa.