SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeunga
mkono kauli iliyotolewa jana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya
Mrisho Kikwete ya kuzitaka timu za ligi kuu kuiga mfano wa Azam kwa kuhakikisha
zinaanzisha timu za vijana na kuwa na viwanja vyao.
Rais Kikwete aliyasem hayo wakati akizindua
uwanja wa kisasa unaomilikiwa na timu ya soka ya Azam Fc ulipo Chamazi, Mbagala
jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo, Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema kwamba,
kwa muda mrefu TFF imekuwa ikivihimiza vilabu hivyo kufanya hivyo lkini
vimekuwa haviutuilii mkazo suala hilo.
Alisema wanashukuru Rais kikwete ameliona hilo
na kulikumbushia kwa mara nyingine hivyo TFF inaamini viongozi wa vilabu husika
watalipa kipaumbe suala hilo.
“Tunapongeza kauli ya Kikwete kwani kwa muda
mrefu tumekuwa tukisisitiza timu kuwa na timu za Vijana pamoja na viwanja vyao
lakini utekelezaji wake umekuwa mdogo,”alisema Osiah.
Kati ya timu 14 zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom ni Azam na
Mtibwa Sugar pekee zenye viwanja hai ambavyo vinaweza kutumika kwa michezo ya
ligi hiyo, huku timu kama Yanga ina walau uwanja wa kufanyia mazoezi.
Aidha, kwa upande wa timu za vijana timu zote
zinazoshiriki ligi hiyo zinamiliki timu za vijana isipokuwa ni timu chache
ikiwemo Azam, Mtibwa Sugar, Yanga na Simba ndizo zinazotilia mkazo kuwekeza kwa
timu za vijana.

Post a Comment