Iringa
imeanza kwa kishindo michuano ya Copa Coca-Cola kwa watoto wenye umri chini ya
miaka 15 baada ya leo (Septemba 3 mwaka huu) kuitandika Ruvuma mabao 4-0.
Hadi
mapumziko katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Shule ya Sekondari Iyunga
jijini Mbeya, washindi walikuwa mbele kwa mabao 2-0 yaliyofungwa dakika ya 14
na Justin Luvanda huku Alphonce Kalinga akifunga la pili dakika ya 43.
Mabao
mengine yalifungwa na Juma Rogani katika dakika ya 49 na Luvanda akafumania
tena nyavu dakika ya 59.
Hiyo ni
mechi ya pili mfululizo kwa Ruvuma kupoteza ambapo ya kwanza ililala mbele ya
wenyeji Mbeya kwa mabao 3-0.
Boniface
Wambura
Ofisa habari
TFF