Na Dina Ismail
EMMANUEL Okwi , nyota wa kimataifa wa Uganda aliyevunja
mkataba na klabu ya Sonderjyske ya Denmark, yuko mbioni kurejea katika klabu
yake ya zamani ya Simba.Jina la Okwi limekuwa likichomoza mara kwa mara klatika
kipindi cha usajili wa wachezaji Bongo
huku akitajwa zaidi katika klabu ya Simba.Hata kipindi cha usajili wa dirisha dogo, uliomalizika katikati ya Desemba mwaka jana nyota huyo
alikuwa akitajwa kurejea Simba, lakini tatizo likawa katika suala la fedha, pia
hakuwa mchezaji chaguo wa kocha mkuu wa Simba, Joseph Omog.Kwamba, kulikuwepo na msigano baina ya viongozi juu ya suala
la kumrejesha kundini Okwi ambaye alijiunga na Sonderjyke Julai 2015 akitokea
Simba iliyomuuza kwa dola 100,000, ambapo kuna waliotaka arejeshwe na kuna
waliokuwa wakipinga.Klabu hiyo ilitaka ilipwe dola 120,000 na Simba ili imuachie
Okwi, kitu ambacho kiligomewa na Simba kwa
madai kwamba haiwezekani wamnunue kwa bei ya juu zaidi ya waliyowauzia.Pia kulikwa na taarifa za kuwepo kwa ‘ujanjaunja’ uliotaka
kufanywa na kiongozi mmoja wa Simba katika mchajkato huo na ndio maana uongozi
uliamua kuacha na mchezaji huyo na kusajili wachezaji wengine wa kigeni.Lakini baada ya Okwi kuvunja mkataba mapema wiki hii kwa
madai ya kutopewa nafasi ya kucheza katika klabu hiyo, Simba inaonesha iko
tayari kumcrejesha kundini kama mchezaji wake na hasa ikizingatiwa wana udhaifu
katika nafasi ya ushambuliaji.Inaelezwa kwamba Okwi atarejea Simba kama mtoto wa nyumbani,
yaani hatopewa dau lolote kwa sasa zaidi ya kupokea mshahara tu wa mwisho wa
mwezi na posho nyingine ndogondogo.Hata hivyo kwa mujibu wa kanuni za soka za Shirikisho la
soka Tanzania (TFF), itakuwa ngumu kwa Simba kumtumia Okwi katika duru la
mwisho la ligi Kuu bara kwani zoezi hilo lilishafungwa na ligi sasa hivi
inaendelea.Hivyo, Okwi atapaswa kusubiri mpaka msimu usajili wa
wachezaji kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.Kwa upande mwingine, Okwi anataka kurudi Simba kwa mtazamo
wa kuwa mmoja ya wachezaji wa kikosi cha
Taifa ya Uganda, ‘The Cranes’ ambacho kimefuzu kucheza fainali ya kombe la
Mataifa ya Afrika (AFCON). Kwamba, kitendo cha kutoitwa
katika kikosi cha timu ya Taifa kilimuumiza sana kwani , kocha mkuu wa The
Cranes, Mserbia Milutin Sredojevic ‘Micho’ alimshauri nyota huyo kujiunga na timu
za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ili iwe rahisi kumfuatilia kwa ukaribu.Kwa upande mwingine, nyota ya Okwi mara nyingi hung’ara
zaidi pindi anapokuwa na klabu ya Simba
kwani kwa mara ya kwanza
mwaka 2013 simba ilimuuza katika klabu ya E’toile du sahel ya Tunisia kwa dau la dola 300,.000,
kablya ya kuvunja mkataba na watunisia hao
baada ya kushindwa kumlipa mshahara na
kurejea Uganda.Aidha, Okwi alikuja tena Tanzania mwaka 2014 na kujiunga na
mahasimu wa Simba, yanga aliyoicheza kwa msimu mmoja tu kabla ya kurejea tena
Simba na ndipo ikamuuza Sonderjyske ya
Denmark kwa dau la dola 100,000.