Mabondia, Selemani Galile kushoto na Tomasi Mashali wakitazamana kwa usongo wa
kila mmoja kutaka kuchukua mkanda wa ubingwa wa mchezo wa masumbwi wa
Oganaizesheni ya ngumi za Kulipwa Nchini TPBO walipokuwa wakitambulisha mpambano
wao. Dar es Salaam jana, utakaofanyika Apri 9.katikati ni Rais wa Oganaizesheni
hiyo Yasin Abdallah Mwaipaya.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
MABONDIA Selemani Galile na Thomas
Mashali wanatarajia kupanda ulingoni Aprili 9 kuwania mkanda wa ubingwa wa
Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBO) litakalofanyika katika ukumbi
wa Friends Corner, Manzese Dar es Salaam.
Pambano hilo linatarajiwa kuwa kati
uzito wa kg 75 raundi 10 likiratibiwa na TPBO.
Wakitambiana Dar es Salaam
jana, wakati wa kuonyeshwa mkanda huo Galile alisema atahakikisha anafanya
mazoezi ya kutosha ili kuweza kuunyakua mkanda huo kwani anauhakika atauchukua
kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao.
"Mkanda lazima niiuchukue kwani najua
Mashali haniwezi na hataweza kunifanya nisichukue mkanda hivyo najiamini na
mkanda ni wangu," alisema Galile.
Naye kwa upande wake Mashali alisema raundi
10 ndio zitaamua mkanda ni wanani lakini anaimani ataunyakuwa kwani anamazoezi
ya kutosha na bado ataendelea kujifua na kuhakikisha anaibuka
bingwa.
"Ninauwezo, nimejipanga na ninauhakika nitaunyakua mkanda lakini yote
raundi 10 ndio zitaamua nani bingwa," alisema.
Naye kwa upande wake Rais wa
TPBO, Yassin Abdalah alisema mkanda huo ulikuwa wazi hivyo wakaamua kuwaambia
mapromota ambapo alijitokeza Prospa Rweyomamu ambaye ndio ameandaa pambano hilo
hivyo bingwa atakayepatikana ndio utakuwa kwake akisubiri mpinzani
Mbali ya kuwepo na mpambano huo siku hiyo kutakuwa na huuzwaji wa DVD za
Mafunzo ya Mchezo wa Masumbwi wakiwemo mabondia Lenox Lewis, Evander
Holfiled,David Haye, Waldmil Klitichiko,Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roj
Jones na wengine wengi
Zitakuwa zikisambazwa kwa ajili ya
kuwapa mabondia,mashabiki marefarii kutambua sheria na kanuni za mchezo huo
Duniani ambazo zimeandaliwa na Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Nchini,
Rajabu Mhamila Super D Alisema kuwa tangia aanze kutoa mafunzo kwa njia hiyo
watu wengi wameanza kuwa na uwelewa wa mchezo wa masumbwi nchini kwa kutambua
sheria na mambo mbalimbali ya mchezo alisema Super D boxing Coach ambapo mpaka
sasa ameweza kutoa matoleo nane tofauti ya mabingwa wa ngumi Duniani
Akichanganya na mabondia wa Nchini.