TIMU YA TAIFA YA RIADHA KUPAA KESHO PARIS KUSHIRIKI OLIMPIKI 2024


Na Makuburi Ally 


TIMU ya Taifa ya Riadha itakayoiwakilisha Tanzania katika michezo ya Olimpiki Paris 2024, imewasili jijini Dar es Salaam leo Agosti 6 ikitokea kambini jijini Arusha.

Timu hiyo inayoundwa na wachezaji wanne na kocha mmoja, iliwasili majira ya saa kumi jioni kwa ndege, ikitokea jijini Arusha ilikokuwa ikijifua kwa takribani mwezi mmoja chini ya udhamini wa CRDB Foundation.

Kikosi hicho kimefikia hotel ya Blue Sapphire iliyoko Vingunguti, ambapo watapumzika na kesho Agosti 7 alfajiri kitakwea pipa kwenda Paris kutupa karata ya pekee ya Tanzania iliyobaki katika michezo hiyo.

Akizungumza baada ya kuwasili Dar, Kocha wa kikosi hicho, Anthony Mwingereza, amesema kambi ilikuwa nzuri na mazoezi yamekwenda vema, kilichobaki ni Watanzania kuwaombea dua warejee na medali.

Nahodha wa kikosi hicho, Alphonce Simbu, amesema wanakwenda kupambana na kilichobaki ni sala za Watanzania tu.

Timu hiyo inaundwa na Simbu, Gabriel Geay, Jackline Sakilu na Magdalena Shauri, ambao wote watashiriki katika Marathon.

Post a Comment

Previous Post Next Post